Exodus 14:10-15

10 aFarao alipokaribia, Waisraeli wakainua macho yao, wakawaona Wamisri wakija nyuma yao. Wakashikwa na hofu, wakamlilia Bwana. 11 bWakamwambia Musa, “Je, ni kwamba hayakuwako makaburi huko Misri hata umetuleta tufe huku jangwani? Umetufanyia nini kututoa Misri? 12 cHatukukuambia tulipokuwa huko Misri, tuache tuwatumikie Wamisri? Ingekuwa vyema zaidi kwetu kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani!”

13 dMusa akawajibu Waisraeli, “Msiogope. Simameni imara, nanyi mtauona wokovu Bwana atakaowapatia leo. Hao Wamisri mnaowaona leo kamwe hamtawaona tena. 14 e Bwana atawapigania ninyi, nanyi mnatakiwa kutulia tu.”

15 fNdipo Bwana akamwambia Musa, “Kwa nini wewe unanililia? Waambie Waisraeli waendelee mbele.
Copyright information for SwhKC